

Naibu Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Dkt.Doto Biteko akipata maelezo kutoka kwa mkuu wa idara ya wateja wakubwa wa Benki ya Azania Bw. Samson Mahimbi juu ya ushiriki na huduma zitolewazo na benki hiyo Kwa Taasisi za Umma wakati Naibu Waziri Mkuu alipotembelea banda la Benki ya Azania katika mkutano wa wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma (CEO’s & Chairpersons Forum) hii leo jijini Arusha ambapo Benki ya Azania imeshiriki kama mmoja wa wadhamini na mdau mkubwa wa mkutano huo.

“Benki ya Azania tunatambua mchango mkubwa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutoa mazingira bora na wezeshi kwa Taasisi za fedha,hivyo na sisi Benki ya Azania tunaendelea kushirikiana na Taasisi za Umma katika kuwapa huduma Bora za kifedha ili ziweze kufikia malengo waliyojiwekea”,alisema Bw.Mahimbi.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!