Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

GSM Group Yadhamini Mbio za Marathon za Siku ya Afrika 2025

  • 35
Scroll Down To Discover

GSM Group imedhamini mbio za marathon za Siku ya Afrika 2025, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kuenzi Umoja wa Afrika na kuimarisha mshikamano wa bara zima.

Tukio hilo kubwa limefanyika leo tarehe 25 Mei 2025, likihusisha mbio za umbali wa 5KM, 10KM na 21KM, na limevuta washiriki zaidi ya 1,000 wakiwemo maafisa wa serikali, wanadiplomasia, wananchi, pamoja na wanariadha maarufu wa Tanzania.

Mbio hizi ni sehemu ya maadhimisho ya kila mwaka ya Siku ya Afrika, siku inayoadhimisha kuanzishwa kwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) mwaka 1963, ambao sasa ni Umoja wa Afrika (AU).

Kaulimbiu ya mwaka huu inalenga kuimarisha mshikamano wa kikanda, biashara huru, na maendeleo jumuishi kupitia mkataba wa AfCFTA.

Kupitia udhamini huu, GSM Group imetoa huduma ya maji safi ya kunywa kupitia bidhaa yake ya GSM Pure Drinking Water kwa washiriki wote wa mbio hizo.

Udhamini huu unaonyesha dhamira ya kampuni hiyo ya kusaidia shughuli za kijamii, kiafya na kiutamaduni ambazo zina mchango chanya kwa jamii ya Kiafrika.

Kwa kuongezea, GSM Group pia ilishiriki katika shughuli nyingine za kuadhimisha Siku ya Afrika, zikiwemo:
• Mei 17, 2025 – Mchezo wa kirafiki wa mpira wa miguu kati ya timu ya Nje Sports na timu ya Jumuiya ya Kidiplomasia Afrika.
• Mei 23, 2025 – Gala Dinner ya kuwakutanisha wanadiplomasia, viongozi wa serikali na wadau wa sekta binafsi katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam. Mgeni rasmi wa Gala dinner hii alikuwa Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Mh. Thabo Mbeki.

Kwa ushiriki wake katika maadhimisho haya, GSM Group inathibitisha nafasi yake kama mshirika wa maendeleo ya kijamii, mdau mzuri wa michezo na muwekezaji wa juhudi zinazojenga Afrika bora ya baadae.



Prev Post Waziri Mkuu Anadi Vivutio Vya Utalii, Uwekezaji
Next Post Rais Mstaafu Thabo Mbeki Aitaka Afrika Kuwa na Ajenda Yake
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook