MAGAZETI ya Leo Jumamosi 24 May 2025
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema kuwa kuanzia Juni hadi Agosti, 2025 kutakuwa na baridi kali na ya wastani katika mikoa sita nchini.jinsi ya kupata elfu 50 leo.
Pia, maeneo mbalimbali nchini yatashuhudia joto, mvua zisizotabirika na kipupwe, huku athari ikitajwa kuwa ni magonjwa yanayohusiana na hali ya hewa ya baridi kama vile homa ya mapafu na magonjwa ya mifugo.
Taarifa hiyo imetolewa na TMA kupitia tovuti yake, ikiwa ni uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa hali ya joto, upepo na mvua msimu wa Juni hadi Agosti 2025.
Hali ya baridi ya wastani hadi joto kiasi inatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi. Hata hivyo, hali ya baridi ya wastani hadi baridi kali inatarajiwa katika maeneo ya mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Rukwa, Singida na maeneo ya magharibi mwa Mkoa wa Dodoma.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!