
Giza bado limetanda ndani ya CHADEMA; mpasuko uko wazi, lakini hatma ya chama haiko wazi.
Mchambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii wa kipindi cha Front Page cha Global TV, Richard Manyota, anasema kuwa tatizo ni matope wanayopakana makada wao kwa wao.
Manyota anahoji: “Je, ndani ya chama hicho kuna mtu anayeweza kuwasafisha CHADEMA dhidi ya matope hayo na kuwafanya wawe safi na wamoja?”
Anasema, endapo hatakuwepo mtu mwenye nguvu ya kuwaunganisha viongozi na makada wa CHADEMA waliochafuana wakati wa uchaguzi na katika sarakasi zinazoendelea sasa, chama hicho kitapoteza mwelekeo.
Kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa, saa 2:30 – 4:00 asubuhi, usikose kufuatilia mijadala mizito ya kitaifa na kimataifa ndani ya Global TV Online.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!