
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeiomba Jeshi la Polisi kutoa maelezo kuhusu hatma ya wanachama wake 10 waliokamatwa wilayani Kibaha, mkoa wa Pwani.
Kwa mujibu wa taarifa ya chama hicho, wanachama hao walikamatwa wakiwa kwenye kikao cha ndani cha chama na hadi sasa hawajafikishwa mahakamani, wala kupewa dhamana.
CHADEMA imelitaka Jeshi la Polisi kufafanua walipo wanachama hao, kuwapatia dhamana kwa mujibu wa sheria au kuwafikisha mahakamani ili kujibu tuhuma zinazowakabili.
Chama hicho kimeeleza kuwa kitendo cha kuwashikilia bila utaratibu ni kinyume na haki za kikatiba na kinakiuka misingi ya utawala wa sheria.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!