
Timu ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliokuwa wakimuunga mkono Freeman Mbowe imetoa wito kwa wanachama wanaokijiita G55, ambao kwa sasa wamekihama chama hicho, kuacha kuendelea kumzungumzia Tundu Lissu. Wamesema kuwa endapo wameamua kuondoka, basi waondoke kimyakimya kama walivyojiunga, badala ya kufanya mikutano na waandishi wa habari huku wakimzungumzia Tundu Lissu, ambaye sasa ni mwenyekiti wao mpya waliyeamua kuungana naye.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!