

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Jumapili, Agosti 24, 2025, ameshiriki Kongamano la Amani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025 lililofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
Kongamano hilo limewaleta pamoja viongozi wa dini, vyama vya siasa, taasisi za kiraia, vijana na wadau mbalimbali wa amani kwa lengo la kuhamasisha mshikamano wa kitaifa na kudumisha utulivu wa nchi wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.
Katika hotuba yake, Rais Samia amesisitiza dhamira ya Serikali na vyombo vya usalama kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru, wa haki na wa amani, akiwataka Watanzania kuendelea kudumisha mshikamano na mshikikiano bila kujali tofauti za kisiasa.



Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!