

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan keshokutwa Jumapili anatarajiwa kuwaongoza Watanzania, kuaga kitaifa mwili wa Makamu wa Rais wa Kwanza na Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee Cleopa Msuya.
Rais Samia anatarajiwa kuongoza shughuli hiyo ya kuaga kitaifa, ambayo itafanyika katika Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam.
Hayo yameelezwa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa leo Ijumaa alipokuwa akiwasilisha taarifa ya kamati ya kitaifa ya mazishi ya viongozi iliyo chini ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!