Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Chalamila Azungumzia Shambulio la Padri Kitima, Awatetea Polisi – Video

  • 30
Scroll Down To Discover

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ametoa wito kwa Watanzania kuwa na imani na Jeshi la Polisi wakati huu likiendelea na uchunguzi wa tukio la kushambuliwa kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Dkt. Charles Kitima.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Mei 2, 2025 jijini Dar es Salaam, Chalamila alisema baadhi ya watu wameonyesha mashaka juu ya taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi, lakini akasisitiza kuwa ni muhimu wananchi wakawa na subira na kuendelea kuwaamini maafisa wa usalama.

“Wako walio na mashaka juu ya taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi. Nawaomba waendelee kuwa na usikivu mkubwa sana. Kwa wale ambao wameonyesha mashaka, waendelee kuwa na imani kubwa kwamba vyombo vya dola havitamuonea mtu yeyote,” alisema Chalamila.

Aliongeza kuwa wote watakaobainika kuhusika katika tukio hilo watafikishwa kwenye vyombo husika vya sheria na kuchukuliwa hatua stahiki.

“Aliyefanya jambo hili atabainika, na hatua kali zitachukuliwa dhidi yake,” alieleza.

Katika hatua nyingine, Chalamila alilaani vikali tukio hilo na kutaka kuondolewa kwa dhana kwamba serikali au masuala ya kisiasa yana uhusiano na shambulio hilo.

“Wapo wanaojaribu kuhusisha tukio hili na serikali au siasa. Sioni mantiki ya serikali au siasa kufurahia jambo la namna hii,” alisema kwa msisitizo.

Chalamila pia aligusia uhusiano wake binafsi na Padri Kitima, akibainisha kuwa amewahi kufanya kazi chini yake na pia ni muumini wa Kanisa Katoliki, hivyo tukio hilo limemgusa kwa namna ya kipekee.



Prev Post Mkurugenzi Zahara Michuzi atunukiwa cheti cha Mfanyakazi Hodari Mei Mosi Maswa
Next Post Shigongo Atangaza Dira ya Viwanda na Utalii, Akemea Kero ya Maji – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook