
Serikali imeongeza kima cha chini cha mshahra kwa watumishi wa umma kutoka shilingi 370,000 hadi shilingi 500,000, likiwa ni ongezeko la asilimia 35.
Ongezeko hilo limetangazwa na Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani Kitaifa mkoani Singida

“Ninayo furaha ya kuwatangazia kwamba katika kuzidi kuleta ustawi wa wafanyakazi mwaka huu Serikali itaongeza kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa Umma kwa asilimia 35.1″, amesema Rais Samia na kuongeza kuwa
“Nyongeza hiyo itaanza kutumika mwezi Julai 2025…huku ngazi zingine za mshahara nazo zikipanda kwa viwango vizuri kadiri ya namna bajeti itakavyoruhusu”.
Rais Samia ameongeza kuwa kwa upande wa sekta binafsi Bodi ya Kima cha Chini ya Mishahara inaendelea kufanya mapitio ili kuboresha mishahara ya wafanyakazi wa sekta binafsi.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!