

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelaani vikali shambulio dhidi ya Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Dkt. Charles Kitima, lililotokea usiku wa Aprili 30, 2025 katika eneo la Kurasini, jijini Dar es Salaam.
Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho, Bi. Brenda Rupia, CHADEMA limetaja tukio hilo kuwa ni “shambulio la kinyama” linaloashiria mazingira hatarishi kwa viongozi wa dini, wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu nchini.

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!