

Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo amesema hawatamvumilia mtu yeyote ambaye anapotosha kuhusu maendeleo yaliyopatikana chini ya serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Shigongo ameyasema hayo mbele ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mohamed Ally Kawaida aliyefika Jimbo la Buchosa kuzungumza na wananchi kwenye mkutano uliofanyika katika Kata ya Nyehuge, Buchosa.
Shigongo amesema mambo mengi na makubwa yamefanyika Buchosa chini ya Rais Samia na kwamba hawatamvumilia mtu yeyote atakayekwamisha au kupotosha kuhusu maendeleo hayo.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!