Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Waziri Mkuu Majaliwa Aridhishwa na Maandalizi ya Mei Mosi Kitaifa Singida

  • 31
Scroll Down To Discover

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na Maandalizi kuelekea sherehe za siku ya wafanyakazi duniani zitakazofanyika kesho Mei mosi, 2025 kitaifa Mkoani Singida katika Uwanja wa Bombadia

Ameyasema hayo leo Jumatano (Aprili 30, 2025) alipopokea taarifa na kukagua maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe hizo. Mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mheshimiwa Majaliwa ameipongeza kamati inayoratibu sherehe hizo na kuwataka kuhakikisha wanakamilisha maeneo machache yaliyobaki ambayo yanahitaji maboresho.

Awali, akitoa taarifa ya maandalizi hayo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Ridhiwani Kikwete amesema maandalizi yamekamilika kwa kiasi kikubwa na wapo tayari kumpokea Rais Dkt. Samia kwa ajili ya sherehe hizo.



Prev Post Mwenyekiti wa UVCCM Taifa: Shigongo Anashirikiana Vyema na Rais Samia Kuleta Maendeleo Buchosa – Video
Next Post Shigongo: Tupo Tayari Kupambana Na Yeyote Atakayejaribu Kupotosha Maendeleo Ya Buchosa – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook