

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mohamed Ally Kawaida amesema Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo anamsaidia Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwenye jimbo hilo.
Akiwa kwenye ziara Buchosa, kawaida amesema ushirikiano wa Shigongo na Rais Samia, umewezesha kukamilika kwa miradi mingi kwenye jimbo hilo, na kuongeza kuwa asinukuliwe kama anampigia Shigongo kampeni.
Akihutubia mkutano wa hadhara katika Kata ya Nyehunge, Buchosa wilayani Sengerema alikofanya ziara ya siku moja, Kawaida amewahamasisha vijana kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi sambamba na kushiriki kwenye uchaguzi kwa kuwachagua viongozi wanaofaa.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!