Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Yas Yazindua Mnara wa Mawasiliano wa 5G Kinyerezi

  • 20
Scroll Down To Discover

Kampuni ya mawasiliano ya YAS imezindua rasmi mnara wa mawasiliano wa teknolojia ya 5G katika eneo la Kinyerezi – Zimbili, Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, katika hafla iliyofanyika tarehe 28 Aprili 2025 na kuhudhuriwa na viongozi wa Serikali na wakazi wa maeneo ya jirani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa YAS Kanda ya Dar Kusini, Bw. Robert Kasulwa, alisema mnara huo ni sehemu ya mkakati wa Kampuni hiyo wa kusambaza teknolojia ya mawasiliano ya kisasa katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa tangu mwaka 2022 ya kuboresha miundombinu ya mawasiliano.

“ Zaidi ya minara 300 ya 5G imeshajengwa jijini Dar es Salaam pekee, na hii inaonesha dhamira ya dhati ya YAS katika kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma bora za mawasiliano,” alisema Bw. Kasulwa.

Aliongeza kuwa uwepo wa teknolojia hiyo ya 5G katika maeneo ya pembezoni kama Kinyerezi – Zimbili unalenga kuongeza ufanisi katika sekta mbalimbali zikiwemo biashara ndogondogo, elimu, afya na upatikanaji wa taarifa mtandaoni, jambo litakalosaidia wananchi kuinua hali zao za maisha.

“Teknolojia ya 5G inatoa fursa ya huduma za uhakika, zenye kasi ya hali ya juu na zinazoweza kutegemewa, hivyo ni chachu ya maendeleo katika nyanja zote za kijamii na kiuchumi,” alisisitiza.

Uzinduzi huo pia umeelezwa kuwa unaendana na mpango wa kidigitali wa Serikali, unaolenga kuhakikisha teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) inawafikia Watanzania wote ili waweze kushiriki kikamilifu kwenye maendeleo ya taifa.

Katika hotuba yake, Bw. Kasulwa alitumia nafasi hiyo kuishukuru serikali kwa ushirikiano wake na kuahidi kuwa YAS itaendelea kushirikiana kwa karibu na mamlaka mbalimbali katika kujenga taifa lenye mawasiliano ya kisasa na jumuishi.

Uzinduzi wa mnara huo wa 5G unatarajiwa kuleta mapinduzi ya kiteknolojia kwa wakazi wa Kinyerezi – Zimbili na maeneo jirani, huku ukifungua milango ya fursa mpya kwa vijana, wajasiriamali na sekta nyingine muhimu za uzalishaji.



Prev Post Benki ya CRDB Yaibuka Kidedea Maonesho ya Kitaifa ya OSHA 2025
Next Post Mapya! Sakata La Mwijaku Na Wanafunzi Wa Chuo, Penzi La Diamond Na Zuchu -Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook