Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Jk Ashiriki Kutoa Mafunzo Chuo Kikuu Cha Havard Huko Boston Kwa Mawaziri Wa Nchi Zinazoendelea

  • 20
Scroll Down To Discover

Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete yuko mjini Boston, Marekani, ambako anashiriki katika kutoa mafunzo kwa Mawaziri wa Fedha na Mawhttps://globalpublishers.co.tz/aziri wa Mipango kutoka nchi mbalimbali zinazoendelea.

Mafunzo hayo yanafanyika chini ya Mpango wa Uongozi wa Ngazi ya Mawaziri wa Harvard, maarufu kama Harvard Ministerial Leadership Program, unaoendeshwa na Chuo Kikuu cha Harvard.

Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Kikwete ni mmoja wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa Wastaafu walioalikwa kushiriki kama wakufunzi, wakitumia uzoefu wao wa uongozi kuhamasisha na kuwajengea uwezo viongozi wa kizazi kipya.

Mbali na Viongozi Wakuu wa Kitaifa Wastaafu, mafunzo haya pia yanashirikisha Wakuu wa Taasisi za Kimataifa, wawakilishi wa mashirika binafsi, pamoja na mabingwa wa masuala ya sera, uchumi na maendeleo kutoka maeneo mbalimbali duniani.



Prev Post Dkt. Biteko Amwakilisha Rais Samia Uwekwaji Wakfu Askofu Mteule Jimbo La Iringa
Next Post Nkane Afurahia Nafasi Yake Yanga Na Kufunga Bao Katika Muungano Cup
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook