

Dar es Salaam, 27 Aprili 2025: Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania ulio chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo umeandaa Maonesho ya Kitaifa ya Utamaduni na Sanaa yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar.

Maonesho hayo yalianza siku ya Tarehe 24 April 2025 na yataendelea hadi siku ya Tarehe 30/4/2025 ambapo yatafungwa na Mhe. Dkt. Dotto Biteko (Mb) Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati.
Katika maonesho haya nchi jirani na Tanzania nazo zimealikwa kushiriki.

Akizungumza kwenye maonesho hayo Afisa Utamaduni wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo kitengo cha Mfuko wa Sanaa na Utamaduni, Flavian Charamila amesema katika maonesho hayo wamezishirikisha nchi jirani ikiwemo Burundi, Uganda na Kenya ambazo ni kila moja imekuja kuonesha ubunifu wake katika nyanja ya sanaa na utamaduni.

Charamila amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi ili kwenda kujionea bunifu za sanaa na utamaduni kutoka mataifa hayo shiriki kwani kwa upande wetu kama wenyeji maonesho haya yanazidi kuitangza nchi yetu pamoja na vivutio vyake.
Miongoni mwa bidhaa za kuvutia za sanaa na utamaduni viwanjani hapo ni pamoja na mavazi, viatu, vitabu, vyombo vya ndani kama vile sahani, mabakuli, hot pot za kitamaduni na vinginevyo.
HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!