Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Safari ya Afrika Yaanza: Simba na Yanga Wapangiwa Wapinzani CAFCL

  • 11
Scroll Down To Discover

Wawakilishi wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL), Simba SC na Yanga, wamepata wapinzani wao katika hatua ya awali ya michuano hiyo msimu wa 2026/27.

Simba , maarufu kama Wekundu wa Msimbazi, imepangwa kukutana na Mighty Wanderers ya Malawi katika hatua ya awali ya mashindano hayo. Timu hizo mbili zitachuana kutafuta nafasi ya kusonga mbele hadi raundi ya pili ya hatua ya awali kuelekea kuwania kufuzu hatua ya makundi ya CAFCL.

Kwa upande wa mabingwa wa Tanzania, Yanga, imepangwa kukutana na Gaborone United ya Botswana katika hatua hiyo hiyo ya awali.

Timu zote mbili za Tanzania zitaanza kampeni zao kwa kucheza ugenini kabla ya kumalizia michezo yao ya marudiano nyumbani, hatua ambayo inaweza kuwa na umuhimu mkubwa katika kuwania nafasi ya kusonga mbele.

Simba na Yanga sasa zitaanza maandalizi ya safari yao ya kimataifa huku zikilenga kuiwakilisha Tanzania vyema na kufikia hatua za juu katika mashindano makubwa ya klabu barani Afrika.

The post Safari ya Afrika Yaanza: Simba na Yanga Wapangiwa Wapinzani CAFCL appeared first on Global Publishers.



Prev Post Rais Samia na Museveni Washuhudia Makubaliano ya Mradi wa Nishati Tanga
Next Post Video: Chalamila Aagiza Uzio wa Ghorofa Masaki Ubomolewe Papohapo
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook