Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Gwiji Wa Soka Rio Ferdinand Aelekea Dodoma Kwa Treni ya Kisasa ya SGR

  • 45
Scroll Down To Discover

Gwiji wa soka duniani, Rio Ferdinand, ameendelea na ratiba yake hapa nchini ambapo leo Mei 20, 2026 ameelekea jijini Dodoma kwa usafiri wa Treni ya Kisasa ya SGR kwa ajili ya kutembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na vivutio mbalimbali vilivyopo katika jiji hilo.

Katika safari hiyo ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa na ujumbe alioongozana nao.

Ziara hiyo inajumuisha pia kufanya mahojiano maalumu yanayogusia fursa mbalimbali za maendeleo ya soka nchini, ikiwemo uwekezaji, programu za vijana, na namna Tanzania inaweza kunufaika zaidi na uzoefu wa kimataifa katika kukuza vipaji.

 

The post Gwiji Wa Soka Rio Ferdinand Aelekea Dodoma Kwa Treni ya Kisasa ya SGR appeared first on Global Publishers.



Prev Post RC Chalamila Atoa Ahadi ya Donge Nono Kwa Dar City
Next Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO MEI 21, 2026
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook