Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mwigulu Aeleza Mafanikio ya Rais Samia Wakati wa Uzinduzi Soko la Kibakwe

  • 12
Scroll Down To Discover

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Jumamosi (Mei 9, 2026) ameweka jiwe la msingi la ufunguzi wa soko la mazao Kibakwe, katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Mkoa wa Dodoma.

Ujenzi wa soko hilo umelenga kuwawezesha wakulima na wafanyabiashara kupata maeneo rasmi, salama na yenye miundombinu stahiki kwa ajili ya biashara ya mazao yao.

Akizungumza na wananchi baada ya uzinduzi wa soko hilo, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amejitambulisha kuwa kiongozi wa matokeo kwa kutekeleza miradi mbalimbali inayogusa moja kwa moja maisha ya Watanzania

“Mheshimiwa Dkt. Samia ni mtendaji. Ambaye akisema jambo, anatekeleza. Na haya yanadhihirishwa kwa kazi kubwa ambayo imefanyika”

Mheshimiwa Waziri Mkuu amesema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia amefanya kazi kubwa inayowapa heshima Watanzania wote. “Nchi inapopiga hatua, kwa kazi kubwa inayofanywa Rais wetu, inalinda heshima ya uhuru wa nchi”.

The post Mwigulu Aeleza Mafanikio ya Rais Samia Wakati wa Uzinduzi Soko la Kibakwe appeared first on Global Publishers.



Prev Post Rais Samia Atembelea Gereza la Ukonga, Akutana na Wafungwa (Picha + Video)
Next Post Rais Samia Ahitimisha Mafunzo ya Uongozi TCT Ukonga (Picha +Video)
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook