Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

YANGA WAONYESHA TABIA YA MABINGWA, PEDRO AWEKA WAZI MALENGO

  • 9
Scroll Down To Discover

KOCHA Mkuu wa Yanga, Pedro Goncalves, amesema mwanzo wa mchezo wao na Sinba haukuwa mzuri kama walivyotarajia, lakini ameridhishwa na namna timu yake ilivyoonesha mwitikio chanya na kurejea mchezoni kwa nguvu.

Ameeleza kuwa licha ya presha ya mchezo, wachezaji wake waliweza kupambana na kuhakikisha wanapata pointi muhimu.

Goncalves amesisitiza kuwa kikosi chake kilionesha tabia ya ushindani, kujituma na mshikamano mkubwa, hali iliyowasaidia kubadilisha mwelekeo wa mchezo.

Kwa mujibu wake, ari hiyo ndiyo imeendelea kuwa silaha yao muhimu katika kusaka matokeo chanya, hasa wanapokutana na changamoto uwanjani.

“Kuna nyakati ambazo mambo hayawi rahisi, hususan nje ya uwanja, wachezaji wamekuwa wakijibu changamoto hizo kwa njia sahihi, kwa kufanya kazi kwa bidii, kujitoa kwa hali ya juu na kuamini katika malengo ya timu,” amesema Pedro.

Ameongeza kuwa lengo lao ni kuendelea kubaki kileleni huku wakidumisha umoja ndani ya kikosi kwa kuwa ushindani ni mkali, kila mmoja anatakiwa kupambana kwa kila pointi ili kuhakikisha wanabaki kwenye nafasi nzuri hadi mwisho wa msimu.

The post YANGA WAONYESHA TABIA YA MABINGWA, PEDRO AWEKA WAZI MALENGO appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post MBUNGE AMWOMBEA URAI CHAMA, BABA LEVO AGOMEA WAZEE
Next Post HAKUNA ANAYETAKA KUKUTANA NA SIMBA YA BARKER
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook