Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Benki ya Exim kushirikiana na Wizara ya Elimu katika nyanja mbalimbali

  • 19
Scroll Down To Discover

Katika kuendelea kuunga mkono juhudi za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kutekeleza mageuzi makubwa ya elimu nchini, timu ya Benki ya Exim ikiongozwa na Afisa Mkuu wa Fedha Bw. Shani Kinswaga pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi na wa kati Bw. Andrew Lyimo na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Bw. Stanley Kafu ilikutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mheshimiwa Adolf Mkenda.

Kikao hicho kilichofanyika jijini Dodoma, Aprili 27, 2026 kilikuwa na lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Benki ya Exim katika nyanja mbalimbali za maendeleo ya elimu, zikiwemo fursa za ufadhili wa wanafunzi wa elimu ya juu hususan wanaosomea sayansi ya data (Data Science), akili unde (Artificial Intelligence) na sayansi shirikishi.

Majadiliano hayo pia yaliangazia fursa mbalimbali ikiwemo fursa za ufadhili unaoweza kutolewa na Benki hiyo, hususani kwa wanafunzi wa elimu ya juu wanaochukua masomo ya sayansi ya elimu ya data na akili unde.

The post Benki ya Exim kushirikiana na Wizara ya Elimu katika nyanja mbalimbali appeared first on SwahiliTimes.



Prev Post NMB Bags Five National AOSH Awards for Second Year Running
Next Post Kutoka madawati hadi vifaa tiba: NMB yaongeza nguvu sekta za afya na elimu Njombe
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook