Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

ALIYEBEZA CHAMA AJIFUNZE SASA, KIUNGO ATIKISA SIMBA

  • 11
Scroll Down To Discover

LICHA  ya usajili wa kiungo wa Simba, Clatous Chama kubezwa na baadhi ya wadau wa soka, nyota huyo ameendelea kuwaziba midomo kwa vitendo kwa kuonyesha kiwango bora tangu kurejea kwake ndani ya kikosi hicho cha Msimbazi.

Chama alirejea Simba katika dirisha dogo la usajili akitokea Singida Black Stars, hatua ambayo ilizua mijadala kwa baadhi ya wadau waliodai kuwa haikuwa sahihi kwa wekundu hao wa Msimbazi kumrejesha kiungo huyo.

Hata hivyo, nyota huyo ameanza kujibu kwa vitendo uwanjani kwa kuonyesha kiwango kizuri na kuthibitisha kuwa uongozi pamoja na benchi la ufundi la Simba chini ya Kocha Mkuu Steven Barker hawakukosea kumrudisha kundini.

Katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida Black Stars, Chama ameonyesha ubora wake kwa kutoa pasi ya bao la ushindi lililofungwa na Elie Mpanzu, hatua iliyosaidia Simba kuondoka na alama tatu muhimu ugenini.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Chama alisema mafanikio hayo yametokana na wachezaji kufuata maelekezo ya benchi la ufundi na kila mmoja kujitoa kwa nguvu zake kuhakikisha timu inapata matokeo mazuri.

“Hakuna mechi rahisi kwetu, kila timu inapambana kwa nguvu kubwa. Katika mchezo dhidi ya Singida Black Stars tulianza vizuri, lakini baadaye tukaruhusu bao. Hata hivyo tulipambana hadi kufanikiwa kupata ushindi,” amesema Chama.

Ameongeza kuwa lengo lao kubwa ni kuendelea kupambana katika kila mechi ili kuhakikisha wanakusanya alama tatu zitakazowaweka katika nafasi nzuri ya kufikia malengo yao ya kutwaa ubingwa mwishoni mwa msimu.

Chama amesisitiza kuwa ari na mshikamano uliopo ndani ya kikosi cha Simba ni mkubwa, huku kila mchezaji akiwa na hamasa ya kupambana ili kuwapa furaha mashabiki wa timu hiyo na kufanikisha ndoto ya kutwaa taji la ligi.

The post ALIYEBEZA CHAMA AJIFUNZE SASA, KIUNGO ATIKISA SIMBA appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post SINGIDA ALENGA USHINDI DHIDI YA MBEYA CITY
Next Post BARKER AFICHUA SIRI YA MPANZU, DAKIKA ZA MWISHO
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook