
Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Pete Hegseth leo Machi 4, 2026 amethibitisha kuwa manowari ya Marekani imezamisha meli ya kivita ya Iran katika Bahari ya Hindi, takribani maili 25 kusini mwa Sri Lanka.
Kwa mujibu wa Hegseth, manowari ya Marekani ilirusha torpedo iliyolenga meli ya kivita ya Iran ijulikanayo kama IRIS Dena, na kusababisha mlipuko mkubwa uliosababisha meli hiyo kuzama.
Maafisa wa ulinzi wa Sri Lanka wamesema wanamaji 32 waliokolewa kutoka kwenye frigeti hiyo, lakini matumaini yanafifia kwa wanamaji wengine 148 wanaoaminika kupotea baharini.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Sri Lanka pamoja na maafisa wa jeshi la majini wamethibitisha, operesheni za uokoaji zinaendelea, huku juhudi za kimataifa zikitarajiwa kusaidia katika msako huo.

Meli hiyo ilikuwa ikirejea kutoka mazoezi ya kijeshi yaliyofanyika katika bandari ya mashariki mwa India wakati iliposhambuliwa.
Kuzamishwa kwa meli hiyo kunakuja wakati mapigano yamezuka Mashariki ya Kati kufuatia mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran.
The post Marekani Yathibitisha Kuzamisha Meli ya Kivita ya Iran Karibu na Sri Lanka – Video appeared first on Global Publishers.






Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!