Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

SIMBA YAJIAMINI, YATUMA SALAMU KWA MPINZANI

  • 26
Scroll Down To Discover

KUFUATIA ubora waliouonyesha wachezaji wa Simba SC katika mchezo wa Kariakoo Derby, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally, amesema kiwango cha sasa cha timu yao kinawapa matumaini makubwa na kumuweka mpinzani katika wakati mgumu.

Ahmed amesema kikosi cha Simba kimeimarika kwa kiasi kikubwa na sasa kina ushindani wa hali ya juu, amesisitiza kuwa timu yoyote itakayokutana nao italazimika kupambana vilivyo ili kupata matokeo.

Ameeleza kuwa kwa ubora waliouonyesha, si rahisi kwa mpinzani kupata ushindi au hata sare bila kupata msaada kutoka sehemu fulani.

Kauli hiyo ya Ahmed imekuja ikiwa ni mwendelezo wa mjadala ulioibuka baada ya mchezo huo kumalizika kwa sare ya 0-0, kufuatia uamuzi wa mshika kibendera, Kassim Mpanga, kukataa bao la Simba lililofungwa na Selemani Mwalimu kwa madai ya kuotea (offside). Tukio hilo limeendelea kuibua hisia tofauti miongoni mwa mashabiki wa soka nchini.

“Kikosi kinazidi kutia matumaini na kinaweza kufanya makubwa msimu huu. Tunajivunia pakubwa kwa ubora tuliouonyesha. Kwa kiwango kile, mpinzani anatakiwa kujiandaa vizuri zaidi,” amesema Ahmed.

Ameongeza kuwa walichokiona katika Kariakoo Derby kinaonesha wazi kuwa Simba ipo kwenye mwelekeo sahihi, na kwamba ili timu yoyote ipate matokeo chanya dhidi yao, lazima kuwe na kitu cha ziada nje ya uwanja.

Ahmed amewataka mashabiki na wanachama wa Simba kuendeleza mshikamano waliouonyesha wakati wa maandalizi na siku ya mchezo huo, akisisitiza kuwa umoja huo ni silaha muhimu katika safari ya kupunguza tofauti ya alama dhidi ya wapinzani wao.

“Mshikamano tulionyesha katika maandalizi ya Derby na umoja wetu, pamoja na kujituma kwa wachezaji, vinatupa imani kuwa tutafanya makubwa na kupunguza tofauti ya alama na mpinzani wetu,” amehitimisha Ahmed.

The post SIMBA YAJIAMINI, YATUMA SALAMU KWA MPINZANI appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post MBINU ZA SIMBA ZAWATIBUA YANGA, PEDRO AJA KIVINGINE
Next Post MSHAMBULIAJI MTANZANIA ASIMULIA ATHARI IRAN
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook