

Dar es Salaam 24 Aprili 2025: Watanzania na Wanajumuiya ya Afrika Mashariki wametakiwa kuendelea kudumisha amani na hasa kipindi hiki ambacho Taifa la Tanzania linaelekea katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa na Mchungaji Patrick Muthee kutoka nchini Kenya ambao wapo nchini Tanzania kwa mwaliko wa Kwaya ya Gethsemane Group Kinondoni (GGK) kutokea Kanisa la Wadventista Wasabato Kinondoni Jijini Dar es Salaam pamoja na uongozi wa kanisa ambapo wameandaa Wiki ya maombi yakiwemo ya kuliombea Taifa letu la Tanzania amani,upendo na mshikamano.

“Tumekuja nchini Tanzania kuungana na ndugu zetu wa Kwaya ya Gethsemane pamoja na Kanisa Group Kinondoni (GGK)ambapo wameandaa wiki ya maombi mbalimbali ya kuliombea Taifa na kwa wakati huu kuomba amani,Umoja na mshikamano ni kipaumbele chetu kwani tunatambua Watanzania watakuwa na uchaguzi Mkuu mwaka huu.Hivyo tunawaombea wawe na amani.”

Pia Mchungaji Mwangi amesema Tanzania na Kenya wamekuwa na mahusiano ya karibu na undugu wao umekuwepo tangu wakati wanamfukuza mkoloni na kupata uhuru na hiyo imeipatia Kanisa kipaumbele kupeleka injili pamoja na kanisa la Waadventista Wasabato Kinondoni kinondoni na kiongozi wa jumuiya ya Afrika.

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!