Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

NAIBU KAMISHNA MKUU TRA AFUNGUA MAFUNZO YA IDRAS KWA WALIPA KODI DODOMA

  • 48
Scroll Down To Discover

Dodoma

 Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato(TRA) Bw. Mcha Hassan Mcha Tarehe 29 Januari 2026 amezindua rasmi mafunzo ya Mfumo Jumuishi wa Usimamizi wa Kodi za Ndani (IDRAS) kwa walipa kodi Mkoa wa Dodoma, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha matumizi ya mifumo ya kisasa ya kidijitali katika utoaji wa huduma za kikodi.

Akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo hayo, Naibu Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Mcha Hassan Mcha, amesema mfumo wa IDRAS umeleta maboresho makubwa kwa kurahisisha upatikanaji wa huduma za kikodi, ikiwemo mawasiliano ya moja kwa moja kati ya walipa kodi na TRA, upatikanaji wa taarifa za kikodi pamoja na uwasilishaji wa huduma mbalimbali kwa urahisi zaidi.

Amesema mafunzo hayo yamelenga kuwajengea walipa kodi uelewa sahihi wa matumizi ya mfumo wa IDRAS, kuongeza uwazi, ufanisi na usalama katika usimamizi wa kodi, sambamba na kujenga imani na kuhimiza ulipaji wa kodi kwa hiari.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Meneja Msaidizi wa Huduma kwa Walipa Kodi, Bw. John Njau, Meneja wa Upelelezi wa Kodi Kanda ya Kati, Bw. Kighenda Nkalang’ang’o, Meneja wa TNCC Mkoa wa Dodoma, pamoja na Afisa Kodi na Mkufunzi wa Mfumo wa IDRAS, Bw. Laurent Kayega

Katika hitimisho lake, Bw. Mcha Hassan Mcha aliwapongeza walipa kodi wa Mkoa wa Dodoma kwa mwitikio mkubwa na ushiriki wao katika mafunzo hayo, akisisitiza kuwa ushirikiano huo ni msingi muhimu wa kuboresha huduma za kikodi na kuleta maendeleo endelevu ya taifa.



Prev Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO JANUARI 29, 2026
Next Post MAGARI YA HUDUMA YA NMB YAFIKIA 15 YAKICHOCHEA UJUMUISHAJI WA KIFEDHA
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook