Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Video: Mwenyekiti wa Mtaa wa Oysterbay Aeleza Mtego Uliowanasa Wachina

  • 36
Scroll Down To Discover

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay, Mololo Mwaisumo, ameuelezea umma namna walivyofanikiwa kuwaweka mtegoni na kuwanasa raia wawili wa China waliokuwa wakihifadhi maburungutu ya fedha ndani ya chumba wanachoishi.

Akizungumza na Global TV, Mwaisumo amesema tukio hilo lilitokana na ufuatiliaji wa kina uliofanywa kwa ushirikiano wa viongozi wa mtaa na vyombo vya usalama, baada ya kupata taarifa za kiashiria cha uwepo wa shughuli zisizo za kawaida katika eneo hilo.

Ameeleza kuwa viongozi wa mtaa walianza kuwafuatilia watu hao kwa muda, huku wakikusanya taarifa muhimu hadi pale mtego ulipowekwa na kufanikiwa kuwanasa wakiwa na kiasi kikubwa cha fedha kilichohifadhiwa katika chumba walichokuwa wakiishi.

Mwaisumo ameongeza kuwa baada ya kukamatwa, raia hao wa China walikabidhiwa kwa vyombo vya dola na tayari wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, ambako wamesomewa shtaka la uhujumu uchumi.

The post Video: Mwenyekiti wa Mtaa wa Oysterbay Aeleza Mtego Uliowanasa Wachina appeared first on Global Publishers.



Prev Post Mke wa Saidi Fella Awaomba Watanzania na Rais Samia Kumsaidia mume wake – Video
Next Post AFCON 2025: Vita ya Nusu Fainali Yaiva Januari 9 na 10
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook