Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Historia Yaandikwa New York Meya wa Kwanza Mwislamu Aanza Kazi

  • 35
Scroll Down To Discover

Zohran Mamdani ameanza rasmi kazi yake kama Meya wa Jiji la New York, akiahidi kuubadili utendaji wa serikali ya jiji kwa ajili ya wananchi wanaohangaika na gharama kubwa za maisha.

Mamdani, ambaye ni mwanachama wa chama cha Democratic na anajitambulisha kama “mdemokrati wa kijamaa,” aliapishwa muda mfupi baada ya saa sita usiku katika kituo cha treni ya chini ya ardhi kilichoachwa chini ya City Hall—akiwa meya wa kwanza Mwislamu katika historia ya jiji hilo.

Katika kiapo hicho cha usiku wa manane, aliweka mkono wake juu ya Qur’an, ishara iliyotajwa kuwa ya kipekee katika uongozi wa jiji lenye wakazi zaidi ya milioni nane.

Baada ya kufanya kazi kwa sehemu ya usiku katika ofisi yake mpya, Mamdani alirejea City Hall mchana kwa hafla kubwa ya hadhara, ambapo Seneta Bernie Sanders alimsimamia kiapo kwa mara ya pili.

“Kuanzia leo, tutatawala kwa upana na kwa ujasiri. Huenda tusifanikiwe kila mara, lakini hatutawahi kushutumiwa kwa kukosa ujasiri wa kujaribu,” alisema Mamdani mbele ya umati ulioshangilia.

Stori na Elvan Stambuli, Global

The post Historia Yaandikwa New York Meya wa Kwanza Mwislamu Aanza Kazi appeared first on Global Publishers.



Prev Post Video: PM Mwigulu Akagua Athari za Mvua Kidete, Atoa Hakikisho la Serikali
Next Post Nafasi 27 za Ajira kwa Wahudumu wa Maduka Dar, Zipo Hapa leo
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook