Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

United, Chelsea Wabanwa Nyumbani, Arsenal Yaizamisha Aston Villa 4–1

  • 41
Scroll Down To Discover

Ligi Kuu ya England iliendelea kwa hamasa kubwa, na matokeo ya mwisho ya mechi za jana yanaonyesha wazi kwamba msimu huu bado umejaa presha, ushindani na matokeo ya kushangaza.

Kwenye Uwanja wa Emirates, Arsenal ilionyesha ubabe wa hali ya juu kwa kuishushia Aston Villa kipigo cha mabao 4–1, huku Manchester United na Chelsea wakilazimishwa sare wakiwa nyumbani matokeo ambayo yameacha maswali kwa mashabiki wao.

FT: Man United 1–1 Wolves
Zirkzee (27’) aliwapa United uongozi, lakini Krejci (45’) akaisawazishia Wolves kabla ya mapumziko.

FT: Arsenal 4–1 Aston Villa
Gabriel (48’), Zubimendi (52’), Trossard (69’) na Jesus (78’) waliipatia Arsenal mabao muhimu, huku Watkins (90+4’) akipunguza maumivu kwa Villa.

FT: Chelsea 2–2 Bournemouth
Palmer (P, 15’) na Fernandez (23’) waliwapa Chelsea matumaini ya ushindi, lakini Brooks (06’) na Kluivert (27’) wakarejesha Bournemouth mchezoni.

Matokeo mengine:
Burnley 1–3 Newcastle United
West Ham 2–2 Brighton
Nottingham Forest 0–2 Everton

The post United, Chelsea Wabanwa Nyumbani, Arsenal Yaizamisha Aston Villa 4–1 appeared first on Global Publishers.



Prev Post Mtanzania Aliyetoroka Oman Afichua Mazito ‘Nilikuwa Napewa Sambusa, Mshahara Hakuna’” – Video
Next Post Mwaka Mpya Ulinikuta Nikiwa na Hofu ya Kodi na Ada, Hivi Ndivyo Nilivyojipanga
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook