Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mkazi Wa Maswa Ahukumiwa Miaka 30 Jela Kwa Kumbaka Binti Yake Na Kumpa Mimba

  • 24
Scroll Down To Discover

Mahakama ya Wilaya ya Maswa, mkoani Simiyu, imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Daudi Mabele (38), mkazi wa Kijiji cha Kakola, kilichopo Kata ya Shishiyu, wilayani humo.

Mabele amehukumiwa kifungo hicho baada ya kupatikana na hatia kwa kosa la kuzini na binti yake wa kumzaa (jina limehifadhiwa) mwenye umri wa miaka 14, na kumsababishia ujauzito.

Hukumu hiyo imetolewa jana, Aprili 24, 2025, na Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Aziz Khamis, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.

Aidha, Hakimu aliamuru mtuhumiwa huyo kumlipa fidia ya Shilingi 200,000 (laki mbili) kwa mhanga, ambaye ni binti yake wa kumzaa.

Awali, kabla ya hukumu hiyo, Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Maswa, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Vedastus Wajanga, alisoma kosa linalomkabili mshtakiwa mbele ya mahakama.

Alieleza kuwa mshtakiwa alitenda kosa la kuzini na maharimu (mwanaume kujamiana na ndugu yake wa damu), kinyume na kifungu cha 158(1) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16, kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022.
Alisema kuwa tukio hilo lilitokea tarehe isiyofahamika katika mwezi wa Septemba, 2024, majira ya usiku, nyumbani kwa mshtakiwa chumbani kwake, wakati mama wa mhanga (ambaye pia ni mke wa mshtakiwa) alipokuwa ameenda nyumbani kujifungua.

Katika kesi hiyo ya jinai yenye namba 6929/2025, upande wa mashtaka uliwasilisha mashahidi watano, akiwemo mhanga mwenyewe, pamoja na kielelezo kilichosaidia kuthibitisha kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo.



Prev Post Makamu Wa Rais Aondoka Nchini Kumwakilisha Rais Samia Kwenye Mazishi Ya Papa Francis
Next Post Spika Wa Bunge Dkt. Tulia Ackson Awasili Mkoani Pwani Kwa Ziara Ya Kikazi
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook