

Yaoundé, Cameroon – Issa Tchiroma Bakary, mgombea wa upinzani ambaye pia amejitangaza mshindi wa uchaguzi wa rais, amempa Rais Paul Biya na serikali yake masaa 48 kuachilia huru watu wote waliokamatwa baada ya uchaguzi wa Oktoba 12.
Tchiroma ametoa onyo hilo huku akipinga rasmi matokeo ya uchaguzi, akisema Wakameruni watalazimika kuchukua hatua wenyewe iwapo wafungwa hao hawataachiliwa. Hii inajiri baada ya kipindi cha ukimya wake usio wa kawaida kwa siku kadhaa.
Ripoti za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa watu 48 wamepoteza maisha katika ghasia za baada ya uchaguzi, huku Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu ikiripoti kuwa zaidi ya watu 1,200 wamekamatwa.











Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!