

Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imekataa ombi lililotolewa na upande wa Jamhuri la kutaka kuahirishwa kwa siku 14 kwa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, kwa kile walichoeleza kuwa ni sababu za kiusalama.
Ombi hilo liliwasilishwa leo Jumatatu na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tawab Issa, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kusikilizwa.
Baada ya kusikiliza hoja hizo, jopo la majaji watatu likiongozwa na Jaji Dunstan Nduguru lilikataa ombi hilo na kueleza kuwa hakuna sababu za msingi za kuahirisha kesi hiyo, hivyo kesi itaendelea kama ilivyopangwa Jumatano, Novemba 12, 2025, saa tatu kamili asubuhi.











Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!