Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Vigogo watakaohudhuria mazishi ya Papa Fransis wajulikana

  • 18
Scroll Down To Discover

Umati mkubwa unatarajiwa Jumamosi na watu wengi kama 250,000 wanatarajiwa kuhudhuria mazishi ya Papa Francis.

Wakuu wengi wa nchi na familia ya kifalme wamethibitisha kuhudhuria mazishi hayo, wakiwemo Mwanamfalme William wa Uingereza, Rais wa Marekani Donald Trump, Mfalme wa Uhispania Felipe VI na Malkia Letizia na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Viongozi wengine wa kisiasa ambao wametangaza kuwa watahudhuria ni pamoja na:
Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva, Rais wa Poland Andrzej Duda, Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.

Wengine ni Javier Milei, Rais wa Argentina, nchi ya kuzaliwa kwa Papa Francis, Waziri Mkuu wa Uingereza Sir Keir Starmer na Waziri Mkuu wa Italia Giorga Meloni.

Papa Francis, ambaye aliepuka baadhi ya fahari za upapa wakati wa uhai wake, ataendelea kuvunja mila katika kifo. Kihistoria, mapapa huzikwa katika majeneza matatu katika makaburi ya marumaru ndani ya Basilica ya Mtakatifu Petro katikati mwa Vatican.

Papa Francis aliomba azikwe katika Kanisa kuu la Roma la St Mary Meja.
Atakuwa papa wa kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka 100 kuzikwa nje ya Vatican.

Katika wasia wake wa mwisho, Papa Francis pia aliomba azikwe ”bila mapambo maalum” na kwa maandishi tu ya jina lake la papa katika Kilatini: Franciscus.

Mwili wake umehamishiwa katika kanisa la Santa Marta Jumatatu jioni, na nyumba yake kufungwa rasmi, Vatican ilisema.

Kufuatia mazishi hayo, mkutano wa makadinali utafanyika ili kumchagua mrithi. Mkuu wa Chuo cha Makadinali ana siku 15 hadi 20 kuwaita makadinali Roma mara tu Papa atakapozikwa.

Majina kadhaa tayari yameorodheshwa kama warithi wanaotarajiwa, na kuna uwezekano mkubwa wa kuibuka katika siku zijazo.

Stori: Elvan Stambuli | GPL



Prev Post MAGAZETI ya Leo Alhamisi 24 April 2025
Next Post Balozi Nchimbi Kwa Nyerere, Akabidhiwa ’Kifimbo’ Kwa Kukubalika
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook