MAGAZETI ya Leo Alhamisi 24 April 2025
Rais Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa uzinduzi wa toleo jipya la juzuu za sheria zilizofanyiwa marekebisho ni hatua muhimu katika kupambana na matumizi mabaya ya madaraka na kuongeza uwazi katika utawala wa sheria nchini.
Akizungumza Jumatano ya Aprili 23, 2025, Ikulu jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa sheria hizo, Rais Samia amesema kuwa sheria hizo zilizoboreshwa zitaziba mianya ya kisheria ambayo hapo awali ilitumiwa na baadhi ya watu kwa manufaa binafsi, ikiwa ni pamoja na kuchochea vitendo vya rushwa.
“Ile ‘tazama kule, tazama kule’ ya kisheria ili mtu apenyeze yake sasa hakuna. Sheria zimeandikwa upya, zimepangwa vizuri, ziko wazi, zinapatikana kwa urahisi na zinaeleweka kwa wananchi. Hii itapunguza uwezekano wa watu kutenda makosa kwa kisingizio cha kutojua sheria,” amesema Rais Samia.
Rais Samia pia amesisitiza kuwa sheria hizo mpya, ambazo zitaanza kutumika rasmi Julai 1, 2025, zitakuwa nyenzo muhimu ya kuimarisha imani ya wananchi kwa Serikali na kuongeza uwajibikaji miongoni mwa viongozi na watendaji wa umma
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!