
Waziri wa Ulinzi na JKT Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax amesifu Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na Jeshi la Kujenga Taifa kwa kutekeleza kwa vitendo maagizo ya Serikali ya kuacha kutumia Nishati Chafu ya kuni na mkaa katika kupikia na kuanza kutumia nishati safi ya Gesi.
Mhe. Dkt. Tax ametoa pongezi hizo wakati wa ziara ya kikazi katika kikosi cha Msange JKT tarehe 23 Aprili 2025 wakati akikagua utekelezaji na utayari wa kikosi hicho katika matumizi ya Nishati ya Gesi.
Amesema katika vikosi alivyopita kukagua miundo mbinu hiyo, amefurahishwa na uokoaji wa fedha zilizokuwa zikitumika kununua mkaa ambapo kwa kikosi cha Msange walikuwa wakitumia Milioni 15,000,000 kununua mkaa kwa mwezi, walipoanza kutumia Nishati ya Gesi wamekuwa wakitumia si zaidi ya shilingi 4,800,000 kwa mwezi.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!