

Rais Samia Suluhu Hassan amempongeza mwanariadha Alphonce Simbu kwa kushika nafasi ya pili katika mashindano ya kimataifa ya Mbio za Boston.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Rais Samia ameandika:
“Pongezi za dhati kwa Alphonce Simbu kwa kushika nafasi ya pili katika Mashindano ya Kimataifa ya Mbio ya Boston (Boston Marathon). Umefanya kazi nzuri.
“Ushindi wako ni matokeo ya kujituma kwa bidii, maandalizi mazuri, nidhamu yako kuanzia jeshini, kwenye mazoezi hadi kwenye mashindano, ukilibeba kwa heshima ya hali ya juu jina la nchi yetu.
“Endelea kuipeperusha vyema bendera ya Taifa letu.”
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!