

Marekani, kupitia Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio, imetangaza kuwa itajiondoa kwenye mazungumzo ya amani kati ya Ukraine na Urusi ndani ya siku chache zijazo endapo hakutakuwa na dalili za wazi za kufikiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano.
Urusi ilianzisha uvamizi wa moja kwa moja dhidi ya Ukraine mwaka 2022, na imeweka masharti kadhaa kuhusu uwezekano wa kumaliza vita hivyo.
Ingawa serikali ya Trump ilionyesha matumaini mwanzoni kwamba ingeweza kusaidia kufanikisha makubaliano ya haraka, juhudi za kufikia usitishaji wa mapigano bado hazijafanikiwa, huku Washington ikilaumu pande zote mbili kwa kukwamisha mchakato wa amani.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!