
Zoezi la Africa India Key Maritime (AIKEYME) limehitimishwa kwa mafanikio makubwa ambapo Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kamandi ya Jeshi la Wanamaji ikishirikiana na Jeshi la Wanamaji kutoka nchini India na majeshi yaliyoalikwa kupata ujuzi na uelewa wa pamoja.
Lengo mazoezi hayo ya pamoja ikiwa ni kupambana na matishio ya uharamia, usafirishaji haramu wa dawa za kulevya, binadamu na usafirishaji haramu wa silaha na madawa ya kulevya.

Akizungumza wakati wa kufunga zoezi hilo, jana 18 Aprili 2025, jijini Dar, Mkuu wa Utumishi Jeshini, Meja Jenerali Marko Gaguti ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jacob John Mkunda amesema kuwa ni ushirikiano huo umekuwa na mafanikio makubwa kwa nchi shiriki kwa kubadilishana uzoefu.
Gaguti amesema lengo kuu la zoezi hilo ilikuwa ni kujifunza mbinu mbalimbali za kukabiliana na changamoto mbalimbali za majini kama vile uharamia, usafirishaji haramu wa dawa za kulevya, usafirishaji wa binadamu na uharifu mwingine wa baharini.
Gaguti aliendelea kusema; “Zoezi hili limefanyika kwa mafanikio makubwa kwa JWTZ na India ambao ndiyo waandaaji pamoja na washiriki wa nchi zingine tisa zilizoalikwa.
“Zoezi hili lililofanyika katika bahari hii ya Hindi limekuwa muhimu sana na sasa tumepata mafunzo ya pamoja ya kuulinda ukanda wetu wa bahari kwakuwa bahari hii ya Hindi ndiyo kitovu kikubwa cha usafiri katika ukanda wetu huu wa Afrika haswa upande wetu wa Afrika Mashariki mpaka Kusini.
“Kwahiyo tunawashukuru viongozi wetu wa kitaifa, Amiri Jeshi Mkuu, Dk. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu wa India kwa kuwezesha zoezi hili kufanyika hapa Tanzania.
“Hivyo basi Kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi, Jenerali Mkunda niwapongeze wote walioshiriki zoezi hili na ni matumaini yetu ni kuwa yale tuliyojifunza yatasaidia kuufanya ukanda wetu huu wa bahari kuwa sehemu salama”. Alimaliza kusema Meja Jenerali Gaguti.
Ukiachana na JWTZ na India pia zimeshirikishwa nchini tisa zilizopakana na bahari katika ukanda wa bahari ya hindi ikiwemo Kenya, Afrika Kusini, Djibouti, Uganda, Msumbiji, Madagascar, Comoro, Shelisheli, Mauritius ambazo zimekuja na meli za vita na meli za utawala kwenye mafunzo hayo ya kupambana na matishio ya baharini.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!