MAGAZETI ya Leo Jumatano 16 April 2025
Bunge limepitisha bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, taasisi zake na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2025/26 huku Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisema Serikali itaendelea kuhakikisha kuna hali ya usalama, amani na utulivu kipindi chote cha uchaguzi.
Ofisi hizo zimepitishiwa Sh782.08 bilioni katika mwaka huo wa fedha.
Hotuba hiyo ilichangiwa na wabunge 103 lakini Majaliwa akasema mambo mengi atayatolea majibu kwa maandishi.
Akihitimisha hoja hiyo Aprili 14, 2025, Majaliwa alisisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi katika maboresho ya awamu ya pili ya Daftari la Kudumu la Wapigakura ili wapate haki yao kwenye uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwisho.
Majaliwa amesema Serikali iko tayari kushirikiana na vyama vya wafanyakazi likiwamo Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), ili wafanyakazi wapate stahiki zao.
Hata hivyo, wakati wa kupitisha vifungu, hakuna mbunge aliyesimama kuhoji jambo lolote, hivyo vimepita kama vilivyoombwa.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!