
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Gissima Nyamohanga amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika ajali ya gari iliyotokea Bunda mkoani Mara.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Meneja wa Tanesco Mkoa wa Mara na kueleza kuwa mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya DDH wilayani humo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, pia amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa atatoa taarifa kamili baadaye.
Chanzo cha ajali hiyo iliyosababisha pia kifo cha dereva wa mkurugenzi huyo, kinaelezwa kuwa ni dereva wa Toyota Land Cruiser, gari alilokuwemo mkurugenzi huyo, kujaribu kumkwepa mwendesha baiskeli na kwenda kugongana na lori.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!