Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC walishiriki kikamilifu katika zoezi la uchangiaji wa damu, lililofanyika katika ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama, makao makuu ya Kanda ya Mashariki zilizoko Ilala jijini Dar es Salaam. Shughuli hii iliyokuwa sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, ilisimamiwa na maafisa wa uhamasishaji kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama.

Wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom Tanzania PLC, Zinga Yahaya (kushoto), Christina Rodrigues( katikati), na Tariq Lukeko wakishiriki katika zoezi la uchangiaji damu kama sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja. Tukio hilo lilifanyika tarehe 7 Oktoba katika ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama, makao makuu ya Kanda ya Mashariki zilizoko Ilala jijini Dar es Salaam, likisimamiwa na Afisa Mhamasishaji kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Comfort Peter Ng’wash.

Vodacom Tanzania inasisitiza mshikamano na jamii na kuhamasisha kila mmoja kushiriki katika shughuli zinazolenga kuboresha afya na maisha ya wananchi. Zoezi kama hili linaonyesha kuwa kusaidia wengine ni sehemu ya moyo wa huduma bora kwa wateja na jamii kwa ujumla.

The post Kuokoa Maisha Kupitia Huduma: Wafanyakazi wa Vodacom Washiriki Zoezi la Uchangiaji wa Damu appeared first on SwahiliTimes.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!