

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mafunzo hayo ambayo yamefanyika jijini Dar-es-Salaam mapema Leo, Octoba, 10, 2025, Kaimu Katibu mtendaji wa NEEC Bi.Neema Mwakatobe amesema kuwa Kupitia mafunzo hayo,ambayo yamewakutanisha waandishi wa habari,na lengo NJ kuwapa elimu namna wanavyofanya majukumu yao na kuwa vyombo vya Habari ni daraja la kueleza dhamira yake na kufikisha elimu ya uwezeshaji kwa Watanzania wengi zaidi.

Amesema ushirikiano huo utasaidia jamii kupata taarifa sahihi kuhusu kazi na majukumu ya Baraza hilo, pamoja na kuelewa fursa zilizopo za kiuchumi nchini.
“Tunatambua mchango mkubwa wa waandishi wa habari katika kuelimisha jamii hivyo basi Kupitia waandishi wananchi wataweza kujua wapi pa kupata msaada wanapokutana na changamoto za kiuchumi, na namna wanavyoweza kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo,” amesema Bi. Mwakatobe.

Pia amesema ni wajibu wa NEEC kiafahamu wadau wote wanatekeleza shughuli za uwezeshaki na kutoa taarifa kwa umma kuhusu fursa zilizopo ili wananchi wapate taarifa
sahihi za uwezeshaji
Kwa upande wa Katibu wa Chama cha Wafanyakazi katika Vyombo vya habari(JOWUTA) Sulemani Msuya amewashukuru NEEC kwa kutoa elimu hiyo kwa wanachama wao,kwani elimu hiyo itatoa uelewa mpana kwa wanahabari kuhusu majukumu na shughuli zinazofanywa na Baraza hilo.
Amesema JOWUTA Ina wanachama zaidi ya 500 nchini kwa mkoa wa Dar es Salaam Ina wanachama zaidi 150,ameiomba NEEC kuendelea kutoa mafunzo kama hayo kwa wanahanari wa mikoa mingine ili kuendelea kueleimisha umma kwa kutoa taarifa sahihi.

“Tunaishukuru NEEC kwa kutambua mchango wa waandishi wa habari,kupitia warsha hii wanachama wetu watakuwa mabalozi wazuri wa kufikisha taarifa za uwezeshaji kwa wananchi,”amesema Msuya
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!