
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM Oktoba 8, 2025 jijini Mwanza, Mgombea Ubunge wa Viti Maalum (Kundi la Vijana) Ng’wasi Damasi Kamani ametoa wito mzito kwa vijana kulinda amani ya nchi yetu.
Amesema, “Sisi tumezaliwa hapa, vitovu vyetu vimezikwa hapa, na hata tukifa tutazikwa hapa, hatuna nchi nyingine zaidi ya Tanzania.”
Amewataka vijana kutokubali kudanganywa wala kushawishiwa kufanya vitendo vinavyoweza kuhatarisha amani, akisisitiza kuwa vita ya kizazi hiki ni vita ya uzuri dhidi ya ubaya, ya kulinda amani na mustakabali wa taifa letu.
Ifikapo tarehe 29 Oktoba 2025, vijana wa Tanzania wanatakiwa kusimama mstari wa mbele kama mabalozi wa amani, wakimpa kura ya ndiyo Dkt. Samia Suluhu Hassan: Mlinzi wa amani, mshindi wa maendeleo.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!