

Airtel Tanzania Yawatembelea Wateja na mawakala wake Jijini Dar es Salaam Katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2025.
Dar es salaam. Katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja 2025, Airtel Tanzania imewatembelea wateja na mawakala wake walipo maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Ziara hii ililenga kusikiliza maoni ya wateja, kuonyesha ubunifu wa huduma, na kuthibitisha dhamira ya kampuni kupitia kaulimbiu yake ya Mteja Kwanza.

Wakiongozwa na Bwn.Charles Kamoto, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, timu hiyo ilitembelea maeneo ya Tandika, Kariakoo na Mbagala, na kuzungumza na wateja na mawakala ili kuelewa uzoefu wao katika kutumia mtandao wa Airtel.
Mazungumzo haya yalionyesha jinsi huduma na suluhisho za kidijitali za Airtel zinavyorahisisha maisha ya kila siku na kuongeza urahisi wa mawasiliano kwa Watanzania.
Akizungumza wakati wa matembezi hayo Mkurugenzi mtendaji wa Airtel Tanzania Bwn.Charles Kamoto, amesema”
“Wiki hii tulitaka kutoka ofisini, kukutana moja kwa moja na wateja na mawakala wetu, kusikiliza maoni yao, na kuhakikisha huduma zetu zinaendelea kuboreshwa ili kukidhi mahitaji yao.”
Kupitia juhudi hizi, Airtel inathibitisha dhamira yake ya kudumu ya kuwatumikia wateja wake, kuboresha huduma zao, na kuhakikisha kila mteja anahisi kuthaminiwa na kupewa suluhisho zinazorahisisha maisha yao.
Kaulimbiu ya Mteja Kwanza inaendelea kuwa mwongozo wa kila huduma, mradi, na uamuzi unaofanywa na kampuni.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!