Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

BAADA YA KUSHINDWANA NA YANGA….CHIMBO JIPYA LA BALEKE HILI HAPA….

  • 8
Scroll Down To Discover

KUNA uwezekano mkubwa wa straika wa zamani wa Simba na Yanga, Jean Baleke akajiunga na AmaZulu FC ya Afrika Kusini, baada ya kuwepo kwa mazungumzo baina yake na uongozi wa timu hiyo kuhitaji huduma yake.

Taarifa kutoka kwa watu wake wa karibu zinasema kilichobakia ni Baleke kusaini mkataba huo, kwani kila kitu kimekamilia kwa asilimia kubwa endapo kama hakutatokea jambo lingine la kufanya dili hilo lisitiki.

“Kuna asilimia kubwa Baleke akasaini Amazulu FC kwa sababu makubaliano kati yake na uongozi wa timu hiyo yalikuwa yamekwenda vizuri, kilichokuwa kimabakia ni kusaini mkataba,” kimesema chanzo hicho na kuongeza:

“Nje na Amazulu FC kulikuwepo na timu nyingine ambazo zilikuwa zinawinda saini yake za ndani na nje, kikubwa alichokiangalia ni maslahi yake.”

Kwa muda aliocheza Simba alifunga manane akiwa amesajiliwa wakati wa dirisha dogo la msimu wa 2022/23 (manane), akaondoka lile dogo la 2023/24 kwenda kujiunga na Al-Ittihad kisha akajiunga Yanga ambayo imeachana nayo msimu huu akiwa amefunga bao moja.

The post BAADA YA KUSHINDWANA NA YANGA….CHIMBO JIPYA LA BALEKE HILI HAPA…. appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post RECAP: Simba walisusia mchezo makusudi kutoa Somo
Next Post HUYU HAPA WINGA TELEZA KUTOKA AZAM FC ANAYENUKI JANGWANI….ANA BALAA HUYOOO😋😋
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook