
Jeshi la Polisi limemkamata Elia Asule Mbugi almaarufu Dogo Bata, Mnyakyusa, mwenye umri wa miaka 25, mkazi wa Segerea, dereva aliyekuwa akiendesha gari namba T 580 EAE aina TATA daladala, ambaye alitoroka Machi 17, 2025 mara baada ya kusababisha ajali iliyosababisha kifo cha SP Awadh Ramadhani Chico, aliyekuwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Chanika.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa na makachero wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Machi 27, 2025 maeneo ya Mbalizi, mkoani Mbeya.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!