
Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz ameuleta mjadala ulioanzishwa na wadau kwenye mtandao wa X kutaka kujua Alikiba ndio msanii bora wa muda wote??
Anasema Mjadala huo ameona una tija kwa sababu inasaidia watu kuwajua wasanii wao bora wa muda wote katika kiwanda cha Bongo Fleva.
Anasema ukweli ni kwamba ukitaja wasanii wenye mafanikio makubwa zaidi kupitia muziki huwezi kuacha kuwataja Diamond na Alikiba.
Wasanii hawa kila mmoja ana ubora wake na wameweka heshima kubwa sana mwenye kiwanda cha Bongo Fleva na wamekuwa kwenye ushindani wa hali ya juu kwa zaidi ya miaka 10.
Mafanikio yao, Fanbase zao Afrika Mashariki hakuna msanii anawafikia na pia aina ya muziki walioufanya umewagusa watu wengi sana.
Kila mmoja na mengi amkubwa aliyoyafanya ila wanatofautiana.
Msikilize @el_mando_tz kisha nawe toa Comment yako hapo chini na tuambie unakubaliana naye au unapingana naye??
Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!