Dar es Salaam, Tanzania – Jumanne 23 Septemba 2025: Watanzania wanaolipa ada za shule, kujaza mafuta, kufanya manunuzi ya nyumbani au kununua vocha za simu kupitia njia za kidijitali za Benki ya Stanbic sasa watapata fursa ya kipekee. Kupitia kampeni mpya ya Masta wa Miamala, Benki ya Stanbic Tanzania itawazawadia wateja kwa miamala ya kila siku inayotumika kwenye maisha yao.
Kampeni hii ya miezi mitatu inalenga kuongeza matumizi ya njia mbalimbali za Stanbic kuanzia kadi za Visa, ATM na mtandao wa Smart App wenye zaidi ya mawakala 600, benki mtandaoni (internet banking) na USSD *150*29#. Imebuniwa si tu kwa ajili ya kukuza matumizi ya kidijitali, bali pia kuwahamasisha wateja wasiotumia akaunti zao na kuwapa nafasi ya kufurahia urahisi na usalama wa miamala isiyo na fedha taslimu.
Kupitia mpangilio wa zawadi, wateja watanufaika katika ngazi tofauti. Watumiaji wakubwa wana nafasi ya kujishindia hadi TZS 100,000, watumiaji wa kati TZS 50,000, huku akaunti zisizotumika zikipewa hamasa kwa zawadi za TZS 25,000. Ili kila muamala uwe na maana, wateja pia watapata bonasi za papo hapo hadi TZS 300 kwa kila muamala.
“Kuhifadhi fedha benki huwa bora zaidi pale unaporahisisha maisha ya kila siku,” alisema Emmanuel Mahodanga, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Benki ya Stanbic Tanzania.
“Masta wa Miamala ni njia yetu ya kuonyesha kuwa huduma za kidijitali sio tu njia salama na rahisi tu, bali pia zenye manufaa. Tunaposherehekea miaka 30 nchini Tanzania, kampeni hii inaonyesha dhamira yetu ya kudumu ya kutembea na wateja wetu na kuchangia katika safari ya ukuaji wa taifa.”
Avin Ngoo, Meneja Idara ya Mawakala wa Benki ya Stanbic Tanzania, alisisitiza nafasi ya mawakala katika kusogeza huduma karibu na watu.
“Kwa kupitia mtandao wa mawakala, Stanbic inavunja vizuizi vya umbali na gharama kwa kusogeza huduma za kifedha karibu na kila jamii. Kila muamala, hata ule mdogo, ni ishara kwamba wateja wetu ni sehemu ya familia ya Stanbic.”
Akionyesha msisitizo wa benki kwenye huduma za kidijitali, Shabani Mwenda, Kaimu Mkuu wa Uboreshaji wa Huduma Binafsi, alisema:
“Kufanya miamala kidijitali siyo suala la urahisi pekee, bali ni ujumuishi. Iwe ni kupitia kadi, App, USSD, au benki mtandaoni (Internet banking), kila muamala una thamani na unaisaidia Tanzania kusogea mbele kuelekea mfumo wa kifedha salama na wenye uwazi zaidi.”
Akizungumzia faida za kadi, Irene Mutahibirwa, Meneja wa Uimarishaji wa Mahusiano ya Wateja, aliongeza:
“Kadi zinawapa wateja wetu zaidi ya urahisi wa malipo. Zinatoa usalama, kumbukumbu za kifedha, na kujiamini. Kila unapotumia kadi yako, unasogea karibu na mustakabali salama na wa kidijitali.”
Hii ni tofauti na promosheni za kawaida, kampeni hii itavuka zaidi ya njia za benki na kuingia kwenye maeneo ya kila siku ya Watanzania.
Watu mashuhuri wataungana na Stanbic kuwaibukia washindi kwenye maduka makubwa, vituo vya mafuta na maeneo mengine ya umma, na kugeuza miamala kuwa matukio ya kijamii yanayoonyesha athari chanya ya kampeni hii.
Taarifa za washindi zitashirikishwa kwenye majukwaa ya kidijitali ili kuonyesha jinsi tabia za kawaida za kifedha zinavyoweza kuleta zawadi halisi.
Kampeni hii pia inazungumzia kukua kwa matumizi ya malipo ya kidijitali nchini. Kadri Watanzania wengi wanavyochagua njia salama zisizo na pesa taslimu, Masta wa Miamala inaonyesha nafasi ya uongozi wa Stanbic katika kujenga uaminifu, urahisi na upatikanaji kwenye mfumo wa kifedha wa taifa.
Stanbic inaposherehekea miaka 30 nchini Tanzania, benki inasema kampeni hii ni sehemu ya dhamira yake pana ya kusaidia familia, biashara na jamii, huku ikisaidia kujenga sekta ya kifedha ya kisasa na jumuishi inayochangia maendeleo ya taifa.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!