
Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz ameizungumzia kauli ya Producer S2kizzy kujiita Producer bora wa muda wote Afrika Mashariki.
Anasema kuwa ni kweli S2kizzy anajeuri ya kujiita hivyo kwa sababu amefanya ngoma zilizofika level ya juu zaidi mpaka kufika GRAMMY na yeye kutajwa GRAMMY.
Numbers kwenye ngoma alizotengeneza, kupenya Kimataifa zaidi ni kweli hilo hatuwezi kupinga ILA…!
Ngoma hizo zimefanywa na wasanii wenye nguvu sana, kujiita Producer bora maana yake lazima uguse kiwanda kizima cha Bongo Fleva.
Lakini pia hata KENYA, UGANDA ulipopataja pia lazima uwaguse walau hata wasanii watatu uwafanyie ngoma ziwe kubwa level ya TETEMA na KOMASAVA.
@el_mando_tz anaongeza kuwa S2kizzy bado ana Room kubwa ya kuwa mkubwa zaidi kufika Level za Majan kugusa Kiwanda kizima na sio wasanii wachache.
Unakubaliana na @el_mando_tz kwa asilimia ngapi??
Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.
Cameraman & Editor @samirkakaa
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!